WAKAZI WA KASARANI WAANDAMANA KUDAI USALAMA

  • | K24 Video
    56 views

    Wakazi wa Kasarani wameandamana leo na kufunga sehemu ya barabara ya Mwiki–Kasarani wakilalamikia ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama. Wanasema mauaji yanayoendeshwa na magenge yameongezeka na malalamishi yao hayajashughulikiwa ipasavyo. Wanataka vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka.